Tumecheza mechi tatu katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid dhidi ya TRA United (Ligi Kuu), Dodoma Jiji (CRDB Federation Cup) na jana Fountain Gate (Ligi Kuu).
Baada ya timu kurejea wachezaji wamepewa mapumziko na baadae jioni watarejea mazoezini kujiandaa na mchezo dhidi ya Namungo utakaopigwa Aprili, 19 katika Uwanja wa Majaliwa.
Advertisement
Kikosi kinatarajia kuondoka Dar es Salaam Ijumaa kuelekea Mtwara na baadae kwenda Lindi tayari kwa mchezo wa Jumapili.