Simba Sports Club
News

Timu yapewa mapumziko ya siku nne

20 Jan 2025

Baada ya ushindi wa mabao 2-0 tuliopata dhidi ya CS Constantine jana wachezaji wamepewa mapumziko na Ijumaa watarudi mazoezini kujiandaa na mechi ya CRDB Federation Cup dhidi ya Kilimanjaro Wonders.

Mchezo wetu dhidi ya Kilimanjaro Wonders utapigwa Jumapili ya Januari 26 katika Uwanja wa KMC saa 10 jioni ambapo sisi tutakuwa wenyeji.

Advertisement

Baada ya kufanikiwa kutinga robo fainali tukiwa kileleni mwa kundi sasa tunarejesha nguvu zetu kwenye michuano ya Ligi Kuu ya NBC na CRDB Federation Cup.

Back to homepage
Share this story