Kikosi kimeondoka na wachezaji wote ambao tutawatumia kwa ajili ya msimu ujao isipokuwa watano ambao wameitwa timu ya taifa ya Tanzania inayojiandaa na michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).
Wachezaji ambao hawakusafiri na kikosi ni mlinda mlango Aishi Manula walinzi Mohamed Hussein na Kennedy Juma kiungo Mzamiru Yassin na mshambuliaji Kibu Denis.
Advertisement
Timu itakaa Misri kwa takribani wiki tatu kabla ya kurejea nchini Agosti 5 tayari kwa Tamasha la Simba Day.