Simba Sports Club
News

Timu yapaa kuifuata Dodoma Jiji

28 Sep 2024

Mchezo huo ambao utapigwa saa 12:30 jioni katika Uwanja wa Jamhuri tunatarajia utakuwa mgumu hasa ukizingatia tunakutana na timu bora ikiwa nyumbani

Kikosi kimeondoka na wachezaji 22 ambao tunaamini wanaweza kutupatia matokeo chanya ambayo yapo ndani ya malengo yetu.

Advertisement

Katika kikosi kilichosafiri yupo mlinda mlango Aishi Manula pamoja na kiungo mshambuliaji Ladaki Chasambi.

Tutaingia katika mchezo wa kesho tukiwa na morali ya hali ya juu ambayo inachagizwa na ushindi wa mabao 2-0 tuliopata kwenye mechi iliyopita dhidi ya Azam FC.

Back to homepage
Share this story