Simba Sports Club
News

Timu yaingia kambini kujiwinda na Orlando

19 Apr 2022

Baada ya ushindi wa bao moja tuliopata katika uwanja wa nyumbani Jumapili, jana wachezaji walipewa mapumziko na leo kikosi kimeanza mazoezi na kuingia kambini moja kwa moja.

Tumeanza mazoezi mapema kwa kuwa lengo letu ni kuhakikisha tunapata matokeo mazuri ugenini ili kufuzu hatua ya nusu fainali.

Advertisement

Morali ya wachezaji ipo juu na hakuna aliyepata majeraha makubwa katika mchezo wetu wa kwanza tunamuomba Mungu waendelee kuwa salama mpaka katika mechi yetu ya marudiano.

Back to homepage
Share this story