Baada ya mchezo jana dhidi ya Mbeya City wachezaji walipewa muda wa kwenda kukutana na familia zao na leo jioni wamefanya mazoezi Mo Simba Arena kabla ya kuingia kambini moja kwa moja.
Kiungo mkabaji Sadio Kanoute ambaye aliukosa mchezo uliopita kutokana na kupata maumivu yupo fiti na amefanya mazoezi pamoja na wenzake.
Advertisement
Wachezaji wote ambao walikuwepo kwenye kikosi kilichocheza jana wako vizuri na wameshiriki mazoezi hayo.