Simba Sports Club
News

Timu yaingia kambini kujiandaa na Kagera Sugar

24 Jan 2022

Kikosi chetu kimeingia kambini jana kujiandaa na mchezo unaofuata wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Uwanja wa Kaitaba Jumatano, Januari 26.

Mchezo huo ni ule wa kiporo ambao awali ulipangwa kuchezwa Desemba 18 mwaka jana lakini ilishindikana kutokanaa na idadi kubwa ya wachezaji wetu kuuugua ghafla hivyo kusababisha kuahirishwa.

Kikosi kitaendelea na mazoezi leo jioni katika viwanja vyetu vya Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo huo ambao tunaamini utakuwa mgumu.

Advertisement

Meneja wa timu Patrick Rweyemamu, amesema licha ya kushindwa kupata ushindi kwenye mechi mbili zilizopita morali ya wachezaji ipo juu na wako tayari kupambana kuhakikisha tunapata alama tatu.

"Baada ya kurudi kutoka Morogoro jana kikosi kimeingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Jumatano.

"Tunajua utakuwa mchezo mgumu, hatujapata ushindi katika mechi mbili zilizopita na mashabiki wetu wanahitaji furaha kwahiyo tutahakikisha tunawapatia Jumatano," amesema Rweyemamu.

Back to homepage
Share this story