Simba Sports Club
News

Timu yaingia kambini kujiandaa na Ihefu

4 Apr 2023

Mchezo huo ambao tunategemea utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wetu utafanyika katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, Ijumaa Aprili 7 saa 10 jioni.

Katika mazoezi ya leo Wachezaji wote wameshiriki isipokuwa Shomari Kapombe ambaye amepewa mapumziko ya wiki moja baada ya kupata majeraha katika mchezo uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca.

Kiungo mshambuliaji, Kibu Denis ambaye nae alipata maumivu katika mchezo dhidi ya Raja yuko vizuri na ameshiriki mazoezi hayo kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Advertisement

Taarifa njema kwa Wana Simba ni kurejea kwa kiungo mshambuliaji wetu Augustine Okrah

Okrah amerejea kikosini baada ya kukosekana kwa Zaidi ya mwezi kutokana na kuuguza jeraha la kuvunjika kidole Hii Leo Augustine Okrah ameshiriki mazoezi wenzie sanjari na kuingia kambini.

Back to homepage
Share this story