Simba Sports Club
News

Timu yaingia kambini kujiandaa na Azam

20 Feb 2023 By simbasc 357 views
Baada ya mazoezi ya jana kikosi kimeingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC utakaopigwa kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa. Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna yoyote ambaye amepata maumivu yatakayomfanya kukosa mchezo wa kesho. Baada ya mchezo wa juzi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca juzi, jana tumeanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Azam moja kwa moja na lengo ni kuhakikisha tunashinda. Viingilio vya mchezo ni kama ifuatavyo: Mzungo Sh. 5000 VIP B na C na Sh. 10,000 VIP A Sh. 15,000 Kama kawaida mchezo wetu wa kesho utapigwa Benjamin Mkapa saa moja usiku.
Advertisement
Back to homepage
Share this story