Simba Sports Club
News

Timu yafanyiwa vipimo vya COVID-19 Benin

18 Mar 2022

Wachezaji, benchi la ufundi na viongozi walioambatana na timu wamefanyiwa vipimo vya COVID-19 leo jioni saa chache baada ya kuwasili nchini Benin.

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limeweka utaratibu kwa kila timu kufanyiwa vipimo hivyo kabla ya mchezo ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo unaosumbua dunia.

Advertisement

Majibu ya vipimo yatatolewa kesho katika mkutano wa maandalizi (pre match meeting) kama ilivyo kawaida.

Hata hivyo, kabla ya kikosi kusafiri wachezaji, benchi la ufundi na viongozi walifanyiwa vipimo vya COVID-19 na wote walikutwa bila maambukizi ya ugonjwa huo.

Back to homepage
Share this story