Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Amaan

19 Apr 2025

Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na wapo tayari kuhakikisha wanapigania nembo ya klabu na kuiwezesha timu kutinga fainali.

Benchi la ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids limewasisitiza wachezaji kutumia nafasi zitakazokuwa zinapatikana katika muda mwingi wa mazoezi ya leo.

Advertisement

Ni mchezo muhimu kwetu ambao tunahitaji kushinda kwa idadi kubwa ya mabao ili tutakapoenda Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya marudiano tuwe kwenye nafasi nzuri.

Back to homepage
Share this story