Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho tayari kwa Derby

12 Aug 2023 By simbasc 161 views
Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Kituo cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jioni tayari kwa mchezo wa Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya watani wetu wa jadi Yanga utakaopigwa kesho. Wachezaji wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na wapo tayari kwa mchezo huo ambao utakuwa na upinzani mkubwa. Mchezo dhidi ya Yanga utakapigwa katika Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga saa moja usiku.
Advertisement
Back to homepage
Share this story