Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho Sokoine

4 Oct 2023

Mazoezi hayo ambayo yamesimamiwa na Kocha Mkuu, Roberto Oliviera 'Robertinho' na wasaidizi wake yamefanyika katika Uwanja wa Sokoine ambao tutautumia kesho kwenye mchezo.

Wachezaji wote 22 tuliosafiri nao wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na hakuna aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa kesho.

Advertisement

Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja ameonyesha jitihada mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi ya kucheza kesho.

Ingawa tunafahamu utakuwa mchezo mgumu na tunaiheshimu Tanzania Prisons lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kuchukua pointi tatu ugenini.

Back to homepage
Share this story