Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho Singida

8 Nov 2022

Kikosi kimewasili jana usiku kikitokea Dodoma kwa usafiri wa basi baada ya kupaa kutoka Dar es Salaam ambapo wachezaji wamepata muda wa kupumzika na leo wamefanya mazoezi ya mwisho.

Wachezaji wote 22 ambao tumesafiri nao wapo kwenye hali nzuri na hakuna yoyote ambaye amepata maumivu na atakosekana kwenye mchezo wa kesho.

Advertisement

Kiungo Clatous Chama ambaye tupo naye kikosini hatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho kutokana na kufungiwa mechi tatu na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi ya Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).

Tutaingia kwenye mchezo wa kesho tukiwa tunajua tunaenda kukutana na timu yenye wachezaji bora na benchi la imara la ufundi lakini tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata alama tatu ugenini.

Back to homepage
Share this story