Simba Sports Club
News

Timu yafanya Mazoezi ya mwisho Sheikh Amri Abeid

8 Apr 2026

Wachezaji wote 26 tuliosafiri nao wapo kwenye hali nzuri wakiwa na ari na morali ya hali juu tayari kwa mchezo huo ambao ni muhimu kwetu kupata alama tatu.

Mchezo dhidi ya TRA utakuwa mgumu na tunatarajia ushindani mkubwa lakini tumejiandaa na tupo tayari kupambana mpaka mwisho ili kupata alama tatu ugenini.

Advertisement

Tutaingia kwenye mchezo wa kesho tukiwa na kumbukumbu ya sare ya bila kufungana tuliopata ugenini dhidi ya Azam FC Jumapili iliyopita.

Back to homepage
Share this story