Wachezaji wote 26 tuliosafiri nao wapo kwenye hali nzuri wakiwa na ari na morali ya hali juu tayari kwa mchezo huo ambao ni muhimu kwetu kupata alama tatu.
Mchezo huu unatukumbusha sare ya bila kufungana tulipokutana mara ya mwisho katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Februari 25 katika dimba la Jamhuri Dodoma.
Advertisement
Tutaingia kwenye mchezo wa kesho tukiwa na kumbukumbu ya sare ya bila kufungana tuliopata ugenini dhidi ya TRA United Alhamisi iliyopita.