Simba Sports Club
News

Timu yafanya Mazoezi ya mwisho New Amaan

28 Feb 2026

Wachezaji wote tuliosafiri nao wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri na hakuna ambaye atakosekana kutokana na kupata maumivu.

Katika mazoezi hayo kila mchezaji ameonekana kuonyesha jitihada kubwa akiwa na ari ya hali juu tayari kwa mchezo huo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa.

Advertisement

Kocha mkuu Steve Barker na wasaidizi wake wamekuwa wakiwasisitiza wachezaji kuwa watulivu na kutokuwa na presha badala yake wajiamini kwakuwa wana uwezo mkubwa wa kuiwezesha timu kupata ushindi.

Back to homepage
Share this story