Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho Morocco

27 Apr 2023 By simbasc 220 views
Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja Kharma kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca utakaopigwa kesho Ijumaa. Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri kamili kwa mchezo wa kesho ambao tunaamini utakuwa mgumu. Aidha, muda wa mchezo wetu utakaopigwa Uwanja wa Mohamed wa V umebadilika kutoka saa moja hadi saa mbili ambapo nyumbani Tanzania itakuwa saa nne usiku.
Advertisement
Back to homepage
Share this story