Mazoezi hayo yamesimamiwa na Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha pamoja na wasaidizi wake ambapo wachezaji wote wameshiriki.
Baada ya mazoezi wachezaji watapumzika kwa saa chache kabla ya kuanza safari ya kuelekea Morocco ambapo watapitia Doha Qatar na kubadili Ndege hadi Casablanca na baadae kubadili tena hadi Marrakech ambapo mechi itafanyika.
Advertisement
Kikosi kinatarajia kuondoka na nyota 23 ambao tunaamini wataweza kutupatia matokeo chanya katika mchezo huo.