Simba Sports Club
News

Timu yafanya Mazoezi ya mwisho Mo Arena

6 Dec 2025

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri huku morali yao ikiwa juu kuhakikisha alama tatu muhimu zinapatikana.

Pamoja na ugumu ambao tunatarajia kuupata kutoka kwa Azam lakini malengo yetu ni kupatikana kwa alama tatu.

Advertisement

Mara zote mechi dhidi ya Azam haijawahi kuwa nyepesi lakini kikosi kipo tayari na wachezaji wanafahamu umuhimu wa alama tatu ambazo zitaongeza furaha kwa mashabiki.

Tutaingia katika mchezo wa kesho tukiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-0 tuliopata katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City siku ya Alhamisi.

Back to homepage
Share this story