Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuenguliwa kwenye kikosi kitakachosafiri kesho.
Tunatarajia kuondoka na wachezaji 23 ambao tunaamini wataweza kufanya kazi kubwa ya kuisaidia timu kufuzu nusu fainali.
Advertisement
Msafara wetu utakuwa na takribani watu 50 hadi 60 ambao utaondoka na Ndege ya Shirika la Ndege la Misri ambapo itasafiri moja kwa moja hadi Cairo.