Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho Mo Arena

30 Dec 2023

Kikosi kilirejea mazoezini Disemba 27 baada ya mapumziko ya sikukuu ya Krismasi na sasa kipo tayari kwa michuano hiyo.

Wachezaji wote isipokuwa walioitwa timu za Taifa kwa ajili ya michuano ya AFCON tunatarajia kusafiri nao kwa ajili ya michuano hiyo ambayo tumepangwa kundi B pamoja na timu za JKU, Singida Fountain Gate na APR ya Rwanda.

Advertisement

Mchezo wetu wa kwanza wa michuano hiyo utakuwa Januari Mosi tutacheza dhidi ya JKU saa 2:15 usiku katika Uwanja wa New Amaan Complex.

Back to homepage
Share this story