Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho Mo Arena

11 Mar 2024 By simbasc 260 views
Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Fountain Gate. Mchezo wetu wa kesho utapigwa saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Azam Complex ambao ndio uwanja wetu wa nyumbani kwa sasa. Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo wa kesho. Tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Singida lakini tupo kamili kuweza kuwakabili na lengo letu ni kushinda na kuchukua pointi tatu.
Advertisement
Back to homepage
Share this story