Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho Mo Arena

1 Oct 2022 By simbasc 313 views
Kikosi chetu leo kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji utakaofanyika katika dimba la Benjamin Mkapa saa moja usiku. Morali ya wachezaji ipo juu na wote wamefanya mazoezi tayari kwa mchezo huo ambao tumeupa kipaumbele kuhakikisha tunashinda na kubaki na alama zote tatu nyumbani. Wachezaji watatu Shomari Kapombe na Peter Banda ambao ni majeruhi wao hawajafanya mazoezi kutokana na kuendelea kupata matibabu wakati Pape Sakho amepata msiba. Lengo letu ni kuhakikisha tunapambana kushinda mchezo wa kesho ili kurejea tena kileleni mwa msimamo.
Advertisement
Back to homepage
Share this story