Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho Misri

23 Oct 2023 By simbasc 180 views
Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho jioni kujiandaa na mchezo wa kesho wa marudiano wa African Football League (AFL) dhidi ya Al Ahly. Kikosi kimefanya mazoezi katika Uwanja wa Cairo International ambao tutautumia katika mchezo wa kesho. Wachezaji wote 24 ambao tumesafiri nao wameshiriki kikamilifu mazoezi hayo na hakuna aliyepata changamoto yoyote ambayo itamfanya kuukosa mchezo. Hali ya hewa haitofautiani na jijini Dar es Salaam ni joto ambalo wachezaji wamelizoea hivyo hakutakuwa na changamoto yoyote.
Advertisement
Back to homepage
Share this story