Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho Meja Isamuhyo

14 Feb 2024

Wachezaji wote ambao tumewatumia katika mechi zetu nne za Kanda ya Ziwa wapo kwenye hali nzuri na wameshiriki kikamilifu mazoezi hayo tayari kwa mchezo wa kesho.

Tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa JKT kutokana na kikosi chao kuwa na nyota wengi wenye uzoefu lakini hata hivyo tumejipanga kuhakikisha tunapambana na kupata ushindi.

Advertisement

Kiungo mshambuliaji Willy Onana ndiye pekee ambaye tutamkosa kutokana nakuwa majeruhi ambayo yatamuweka nje kwa takribani wiki moja.

Back to homepage
Share this story