Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho Levy Mwanawasa

15 Sep 2023 By simbasc 172 views
Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Levy Mwanawasa tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Power Dynamos. Kwa mujibu wa kanuni ya Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) timu mgeni anatakiwa kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi ili kuzoea hali ya uwanja. Wachezaji wote 24 ambao tumesafiri nao wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata maumivu yoyote ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa kesho. Tutaingia kwenye mchezo wa kesho kwa kuwaheshimu Power Dynamos lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda.
Advertisement
Back to homepage
Share this story