Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho kwa Mkapa

21 Apr 2023

Kiungo mkabaji Sadio Kanoute ambaye alikuwa majeruhi na amekosa mechi kadhaa zilizopita amerejea na ameshiriki mazoezi hayo na yuko tayari kuipambania timu kesho.

Kama Kocha Roberto Oliviera 'Robertinho' na wasaidizi wake kama wataona inafaa watatumia kiungo huyo kwenye mchezo wa kesho kwa kuwa yuko tayari.

Advertisement

Wachezaji wetu wote wameshiriki kikamilifu mazoezi hayo isipokuwa mlinda mlango, Aishi Manula ambaye hayupo fiti asilimia 100 wengine wote morali ipo juu tayari kuhakikisha wanafanya kila linalowezekana kupata ushindi wa nyumbani kesho.

Ingawa tunafahamu mchezo utakuwa ngumu na tunaiheshimu Wydad kutokana na ukubwa wake na historia yake lakini tupo tayari kuwakabili na kuwapa furaha Wanasimba.

Back to homepage
Share this story