Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho kwa Mkapa

19 Oct 2023

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na hakuna ambaye amepata maumivu yatayomfanya kuukosa mchezo wa kesho.

Mlinzi wa kati Henock Inonga ambaye amerejea nchini usiku wa kuamkia leo kutoka DR Congo alipokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa nae ameshiriki mazoezi hayo na yupo tayari kwa mchezo wa kesho.

Advertisement

Tutaingia kwenye mchezo wa kesho kwa lengo moja la kuhakikisha tunapambana kupata ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri katika mechi ya marudiano itakayopigwa Cairo, Misri Oktoba 24.

Tunawaheshimu Al Ahly kutokana na ubora na uzoefu wake kwenye michuano ya Afrika lakini tupo tayari kuhakikisha tunapata matokeo chanya.

Back to homepage
Share this story