Mchezo huo utapigwa Jumapili saa moja usiku ambapo timu inaondoka mapema ili kupata nafasi ya siku mbili kufanya mazoezi na wachezaji kuzoea hali ya hewa.
Meneja wa timu, Patrick Rweyemamu amesema tutasafiri na kikosi cha wachezaji 25 tukiwa na lengo la kutafuta alama tatu muhimu ugenini.
Advertisement
"Kikosi kimefanya mazoezi ya mwisho asubuhi na tutasafiri saa tisa alfajiri kuelekea Benin ambapo mechi yetu dhidi ya ASEC itachezwa.
"Tunasafiri na Ethiopia Airline tukiwa na kikosi cha wachezaji 24 na lengo letu kama timu ni kuhakikisha tunashinda ugenini," amesema Rweyemamu.