Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata majeraha yoyote ambayo yatamfanya kukosa mchezo wa kesho.
Benchi la ufundi limeendelea kuwasisitiza wachezaji umuhimu wa ushindi katika mchezo wa kesho kwakuwa tunaelekea katika mechi za makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Advertisement
Tunafahamu Singida ni miongoni mwa timu zilizosajili vizuri msimu huu na ina benchi bora la ufundi lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda hasa tukiwa katika Uwanja wa nyumbani.
Ushindi kwenye mechi ya kesho itatuongezea morali kuelekea mchezo wetu wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya ya Guinea utakaopigwa ugenini Februari 12.