Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na Mtibwa

16 Aug 2023 By simbasc 182 views
Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Highland Morogoro kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Manungu Complex saa 10 jioni. Morali za wachezaji zipo juu na wapo tayari kuhakikisha tunapambana kuhakikisha tunaanza kwa kupata alama tatu nyumbani. Mchezo wa kesho ni wa kwanza wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC 2023/24 na malengo yetu ni kuanza kwa ushindi.
Advertisement
Back to homepage
Share this story