Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na Mbeya City kesho

22 Nov 2022

Wachezaji wote 22 waliosafiri wamefanya mazoezi hayo na jambo jema ni kwamba hakuna aliyepata majeraha hivyo Kocha Juma Mgunda atakuwa na wigo mpana wa kupanga kikosi chake.

Morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja ameonyesha jitihada zake mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi kesho.

Advertisement

Tunafahamu utakuwa mchezo wenye upinzani mkubwa lakini tumejiandaa kikamilifu kuhakikisha tunashinda na kuondoka na alama zote tatu.

Back to homepage
Share this story