Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na Jamhuri

7 Jan 2024 By simbasc 351 views
Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa nje wa New Amaan Complex kuikabili Jamhuri katika mchezo robo fainali ya michuano ya Kombe Mapinduzi utakaopigwa kesho saa 2:15 usiku. Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata maumivu ambayo yanaweza kumfanya kuukosa mchezo wa kesho. Morali za wachezaji zipo juu na tutaingia kwenye mchezo wa kesho tukiwa na lengo la kuibuka na ushindi ili tutinge nusu fainali. Tayari kocha msaidizi, Seleman Matola ameweka wazi kuwa haitakuwa mechi rahisi na tunategemea kupata upinzani lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo chanya.
Advertisement
Back to homepage
Share this story