Mchezo huo utapigwa saa moja usiku katika Uwanja wa Azam Complex na sio Uhuru kama ilivyokuwa imetangazwa awali.
Shomari Kapombe ndiye mchezaji pekee ambaye hakushiriki mazoezi kutokana na kupewa mapumziko ya wiki moja kutokana nakupata maumivu katika mchezo uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca.
Advertisement
Wachezaji wapo kwenye hali nzuri morali zipo juu na wapo tayari kupambana kuhakikisha tunashinda na kusonga mbele hatua ya nusu fainali.
Moja ya lengo letu msimu huu ni kuhakikisha tunashinda taji hili na ndoto yetu itatimia kwa kuanza kushinda mchezo wa kesho dhidi ya Ihefu.