Kikosi kitaondoka kesho kuelekea Abu Dhabi ambako mchezo huo utafanyika na wachezaji wote wameshiriki mazoezi ya mwisho.
Katika hatua nyingine, Kocha Mkuu Roberto Oliviera 'Robertinho' amefurahishwa na jinsi wachezaji wanavyojituma na kushika vizuri mafunzo anayowapa.
Advertisement
Morali ya wachezaji ipo juu wanafanya jitihada mazoezini ili kumshawishi Kocha Robertinho awape nafasi.
Aidha, mshambuliaji Moses Phiri naye ameanza mazoezi mepesi baada ya kupona majeraha yake yaliyomfanya kukosa mechi mbili za mwisho za ligi.