Mchezo wetu dhidi ya African Sports utapigwa katika Uwanja wa Uhuru saa 10 jioni sababu dimba la Benjamin Mkapa ambalo tunalitumia kwa mechi zetu za nyumbani kuwa kwenye ukarabati.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo isipokuwa Kibu Denis ambaye amepata maumivu ya mguu kwenye mchezo wetu uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers na atakuwa nje kwa wiki nzima.
Advertisement
Tutaingia kwenye mchezo wa kesho kwa kuiheshimu African Sports sababu lengo letu ni kuhakikisha tunashinda na kutinga robo fainali.
Tunafahamu mchezo utakuwa mgumu kwakuwa ni mechi ya mtoano hivyo tumejipanga na kuchukua tahadhari zote ili kutimiza malengo yetu.