Kikosi kiliwasili Kigoma leo mchana na wachezaji walipata saa chache za kupumzika kabla ya jioni kufanya mazoezi ya hayo ya mwisho yaliyoongozwa na Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha.
Katika mazoezi hayo hakuna mchezaji aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa kesho.
Advertisement
Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja amejitahidi kuonyesha uwezo wake mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi katika mchezo wa kesho.
Mchezo wa kesho tunaupa umuhimu mkubwa na tunahitaji kupata ushindi ili kufuzu robo fainali kwakuwa moja ya malengo yetu msimu huu ni kutwa taji la michuano hii.