Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho Kaitaba

20 Dec 2022 By simbasc 369 views
Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Kaitaba tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar. Kikosi kimefanya mazoezi kuanzia saa moja usiku kwa kuwa mchezo wetu huo utapigwa muda huo hapa hapa Kaitaba. Wachezaji wote 24 wameshiriki mazoezi hayo na hakuna ambaye amepata majeraha yatakayomfanya kukosa mchezo wa kesho. Tunafahamu mchezo utakuwa mgumu na tunaiheshimu Kagera lakini tutapambana kuhakikisha tunapata alama zote tatu.
Advertisement
Back to homepage
Share this story