Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuivaa Kotoko kesho

27 Aug 2022 By simba 566 views

Kikosi chetu leo kimefanya mazoezi ya mwisho usiku huu katika Uwanja wa Al Hilal kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Asante Kotoko kutoka Ghana.

Kikosi kimewasili hapa Khatoum jana mchana na jioni kilifanya mazoezi ya utimamu wa mwili kutokana na uchovu wa safari.

Advertisement

Wachezaji wote tuliosafiri nao wapo kwenye hali nzuri na hakuna ambaye tutamkosa kutokana na majeruhi.

Mchezo wetu wa kesho utapigwa katika Uwanja wa Al Hilal saa moja usiku ambapo kwa saa za nyumbani itakuwa saa mbili.

Back to homepage
Share this story