Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya mwisho Jamhuri

10 Mar 2023 By simbasc 195 views
Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho jioni katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro tayari kujiweka sawa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar. Wachezaji wote 25 ambao tumesafiri nao wameshiriki mazoezi hayo na jambo jema ni kwamba hakuna aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa kesho. Wachezaji wamejitahidi kufanya jitihada kwenye mazoezi hayo ili kulishawishi benchi la ufundi kuwapa nafasi kwenye mchezo wa kesho. Morali za wachezaji zipo juu na kesho tutaingia kwenye mchezo tukiwa na lengo moja la kupambana kupata alama tatu ingawa tunafahamu haitakuwa mechi rahisi. Mchezo wetu dhidi ya Mtibwa utapigwa kesho katika Uwanja wa Manungu Complex saa 10 jioni.
Advertisement
Back to homepage
Share this story