Wachezaji wote wameshiriki kikamilifu na morali ipo juu kuhakikisha tunashinda na kufufua matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali.
Ushindi katika mchezo wa kesho utakuwa ni wa kwanza kwenye hatua hii ndio maana tumejipanga kuhakikisha tunashinda.
Advertisement
Haitakuwa mechi rahisi kutokana na ubora wa Wydad lakini tupo imara kupambana hadi mwisho ili kuwapa furaha Wanasimba na kubaki na alama tatu nyumbani.
Katika mchezo huo tutakosa huduma ya nyota wetu Saido Ntibazonkiza na Sadio Kanoute ambao wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.