Wachezaji wote 24 tuliokuja nao wameshiriki mazoezi hayo na wamemaliza salama hakuna aliyeumia.
Hali ya hewa ni joto sawa na nyumbani jijini Dar es Salaam kwahiyo wachezaji hawatapata changamoto ya kimazingira kwenye mchezo wa kesho.
Advertisement
Morali ya wachezaji ipo juu na wapo tayari kuhakikisha tunapata alama tatu muhimu ugenini ili kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye kundi letu la C.
Mchezo wetu kesho utapigwa saa 10 jioni kwa saa za Guinea ambapo nyumbani Tanzania itakuwa saa moja usiku.