Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo hivyo kocha Roberto Oliviera 'Robertinho' na wasaidizi wake watakuwa na wigo mpana wa kupanga kikosi.
Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja amejitahidi kufanya jitihada mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi kesho.
Advertisement
Mchezo wetu dhidi ya Vipers utapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kesho saa moja usiku.
Tayari vituo zinapopatikana tiketi tumevitangaza na sehemu zote ambazo tunazunguka na gari la hamasa zinauzwa pia.