Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho ambao tunaamini utakuwa mgumu.
Morali za wachezaji zipo juu na kila mchezaji ameonyesha jitihada kubwa mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi mchezo wa kesho.
Advertisement
Tunawaheshimu Al Ahly kutokana na ubora walionao na historia yao kwenye michuano hii lakini tumejipanga kuhakikisha tunavuka hatua hii.
Tunaendelea kuwaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani kesho ili kuwapa morali wachezaji ili kwa pamoja tutimize lengo la kufuzu nusu fainali.