Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya kwanza nchini Misri

28 Mar 2025

Mazoezi hayo yamefanyika katika viwanja vya Hoteli tuliyofikia ya Tolip Hotel Resort ambapo wachezaji wote wameshiriki.

Nyota sita waliokuwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania waliocheza dhidi ya Morocco siku ya Jumatano walikuwa wakwanza kufika Misri na wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu.

Advertisement

Kwa mujibu wa ratiba kikosi kitaendelea kufanya mazoezi usiku ili kuendelea kuzoea mazingira ya hali ya hewa.

Back to homepage
Share this story