Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi ya kwanza Morocco

7 Dec 2023

Kikosi kiliwasili katika mji wa Marrakech jana ambapo wachezaji walifanya mazoezi ya utimamu wa mwili kwa ajili ya kuondoa uchovu wa safari lakini leo ndio wameendelea na programu ya mwalimu.

Kesho pia kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja huo huo lakini yatakuwa usiku muda ambao mchezo wetu utapigwa.

Advertisement

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo kwa asilimia 100 na wanaonekana wapo tayari kuipigania timu kupata ushindi Jumamosi.

Back to homepage
Share this story