Baada ya kikosi kuwasili hapa Malawi leo saa mbili asubuhi wachezaji na benchi la ufundi walipumzika kabla ya jioni kufanya mazoezi ya utimamu wa mwili.
Wachezaji wote 25 waliosafiri wamefanya mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri.
Advertisement
Kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho kesho saa 10 jioni katika Uwanja wa Taifa wa Bingu ambao utatumika kwa mchezo wa Jumamosi kama kanuni za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zinavyoelekeza.