Simba Sports Club
News

Timu yafanya mazoezi TPC Moshi kujiandaa na Polisi

8 Apr 2022

Kikosi kimewasili Moshi saa 10 jioni kutoka jijini Tanga na saa 12 kimefanya mazoezi ya utimamu wa mwili baada ya mchezo wa jana dhidi ya Coastal Union.

Wachezaji wote waliosafiri wamefanya mazoezi na hakuna aliyepata maumivu kwenye mchezo wetu wa jana.

Advertisement

Kesho kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Ushirika ambao utatumika kwenye mchezo wetu Jumapili saa 10 jioni.

Back to homepage
Share this story