Wachezaji wote waliosajiliwa kwa ajili ya michuano hii wameingia kambini na jioni wamefanya mazoezi tayari kwa maandalizi ya mchezo huo ambao tunauchukulia kama fainali.
Morali ya wachezaji ipo juu na wameahidi kuhakikisha wanajitoa wakati wote wa mchezo ili kupata ushindi ambao utatupa tiketi ya kutinga robo fainali.